Psalms 50:1-6

Ibada Ya Kweli

(Zaburi Ya Asafu)


1 aMwenye Nguvu, Mungu, Bwana,
asema na kuiita dunia,
tangu mawio ya jua
hadi mahali pake liendapo kutua.

2 bKutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu,
Mungu anaangaza.

3 cMungu wetu anakuja na hatakaa kimya,
moto uteketezao unamtangulia,
akiwa amezungukwa na tufani kali.

4 dAnaziita mbingu zilizo juu,
na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake:

5 e“Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu,
waliofanya agano nami kwa dhabihu.”

6 fNazo mbingu zinatangaza haki yake,
kwa maana Mungu mwenyewe ni hakimu.

Copyright information for SwhKC